Alhamisi, 8 Agosti 2013

Obama aahidi Kenya msaada kuhusu JKIA

Ndege za kimataifa zimeanza kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa jijini Nairobi JKIA, siku moja tu baada ya kitengo cha kuwasili wageni kuchomwa na moto mkubwa.
Ndege ya kwanza ya kimataifa kuwasili katika uwanja huo ni ile iliotoka Uingereza na baadaye nyengine kutoka Tanzania na Bangkok zikawasili.
Wachunguzi hata hivyo wanatafuta mabaki ya moto huo ili kutathmini chanzo chake.
Wakati huo huo Rais wa Marekani, Barack Obama amesema ataisaidia serikali ya Kenya katika kukarabati uwanja huo wa ndege baada ya moto mkubwa kuuteketeza hapo jana.
Katika ujumbe wake wa simu, Obama alisisitiza kuwa Marekani iko tayari kuisadia Kenya katika hali ile yoyote kutokana na ushikiano wake na Kenya.
Obama pia aliwapa pole familia zilizowapoteza wapendwa wao katika mashambulizi ya bomu ya Agosti 1998 mjini Nairobi.
Manmo Jumatano, moto mkubwa uliotokea majira ya asubuhi, uliharibu kitengo cha kuwasilia wageni wa kimataifa.
Vikundi vya wachunguzi viliwasili katika uwanja huo kufanya uchunguzi wao kubaini kilichosababisha moto huo.
Abiria walikwama kutokana na mkasa huo ingawa waliweza kuondolewa nje ya uwanja kwa ajili ya usalama wao huku baadhi wakiangalia mizigo yao ikiteketea wasijue la kufanya. .
Rais Uhuru Kenyatta aliwasili katika uwanja huo na kujionea uharibifu uliotokea na kiisha kutoa taarifa yake kupitia kwa msemaji wake Esipisu aliyesema kuwa chanzo cha moto huo kinachunguzwa.

Wema Sepetu ATEMBELEWA NA WASHIRIKI WA BIBI BOMBA OFISINI KWAKE LEO

Wema akiwakaribisha Bibi Bomba...
 Mchana wa leo CEO wa kampuni ya Endless Fame Production... Wema Sepetu alipata ugeni kutoka kwa washiriki wa Bibi Bomba (2013)...Kipindi kinachorushwa hewani na Clouds Tv The People Station kikiongozwa na Babuu wa Kitaa... Mabibi wanne walioonekana kuwa na uwezo katika fani ya maingizo walipata nafasi yakujifunza baadhi ya mambo muhimu katika Tasnia nzima ya maigizo...


Darasa likaanza sasa....
Maswali na majibu nayo yalikuwepo....
Babuu wa Kitaa akifanya yake...

Baada ya kutoa mafunzo Wema alitoa nafasi kwa baadhi ya Mabibi kuonesha uwezo wao kwakile walichojifunza... Pichani ni Bibi akionesha uwezo wake kwakucheza kama Boss wake Wema na Wema akicheza kama mwajiriwa wake...



Bibi mwenye nguo ya rangi ya zambarau alioneshesha uwezo wake alipoambiwa amwage chozi baada ya kupewa taarifa kutoka kwa mfanyakazi wake wa ndani kuwa amemuona mumewe akiwa Bar na mwanamke mwingine.... LOL!_






Picha ya pamoja....

Jumatatu, 5 Agosti 2013

BAD LUCK COMING SOON

Ile Sinema iliomshirikisha miss Tanzania mwaka jana Salha Israel, Muda si mrefu itaingia mtaani kwa kishindo inayokwenda kwa jina la BAD LUCK Wadau mzigo huu si wa kuukosa kama kawaida ya RJ Company uwa hawabahatishi kwenye kazi.

Staff wa RJ COMPANY wakiwa kwenye pozi kabla kazi kuanza..


   Maandalizi yakianza kwa ajili ya kuupika mzigo wa BAD LUCK ambayo kwa sasa ushakamilika kwa kuingia sokoni.

Baba Haji na Johari on set hatari sana mzigo huu wadau..

Lisa pia alikuwepo maarufu kwa jina la Batuli naye yuko ndani ya mzigo wa BAD LUCK.

 Director Adam Kuambiana.

Nami pia nilipita kuwaangalia vijana wangu wakifanya kazi kipindi hicho.....

   Batuli bila kukosa ndani ya nyumba ni hatari sana..



 Miss akifanya mambo yake kwenye Bad Luck.

  Batuli na Johari wakiwa On Set..

  Kazi ni ngumu sana Location. Wakati mwingine kunakuwa na kazi ngumu sana maana sio kazi ndogo kabisa tutieni moyo   msituvunje moyo mapambano bado yanaendelea..

Uwoya alipita location kuangalia jinsi RJ COMPANY wanavyofanya kazi.

 Vijana kazini....

Esha Buheti on Set...

CHECK OUT: BIKINI, SIDIRIA NA VITUMBO NJE NJE!


Just because you are late stage pregnant doesn’t mean you can’t dress in a bikini, so that is just what dozens of women did.

About forty pregnant women, all in their third trimester, competed in Houston, in the Annual Pre-Labor Day Pregnant Bikini Contest.

The ladies proved their parenting skills in challenges such as changing baby's diaper before throwing and strutting down the runway to show their punches. The contest gives fun loving women a chance to show off their
incredible bodies capable of growing a whole separate life. While women compete, their families, friends and associates encourage them.

Jennifer Clay, who is in her 32nd week of pregnancy, was

deemed the winner based on her grace, presentation and an "it" factor.

The event, organized by a radio program held in Grand Woodrow, is in its eighth year, but has not escaped controversy with some bloggers who criticize the practice. "So, I'll just come right out and say it: I have mixed feelings about this," writes Jacqueline Burt on the contest last year. "Look, I'm all for self-acceptance and have a positive body image regardless of size or shape, but a pregnant bikini contest? I just do not know if I agree with that."!

MCHEKESHAJI MAARUFU WA ZE COMEDY EATV AFIWA NA KAKA YAKE KUPITIA AJALI YA GARI JIJINI DAR ES SALAAM LEO! SOMA HAPA

MSANII Mchekeshaji maarufu hapa nchini kutoka kundi la Ze Comedy kipindi kinachorushwa na runinga ya EATV Channel 5 ''Mtanga mtangalile'' Leo amefiwa na kaka yake kwa jina ''Azizi'' baba mmoja mama mmoja, Kwa mujibu wa mtu wa karibu habari iliifikia Masai Nyotambofu Blog kwamba
alifariki kwa ajali Jijini Dar Es Salaam, Habari zaidi kuhusiana msiba huo mtaendelea kuzipata hapa hapa, masainyotambofu.blogspot.com inampa pole Mtanga pamoja na familia nzima kwa ujumla ndugu jamaa na marafiki wote.. R.I.P Brother Azizi.

Zuma ampa hongera kubwa Mugabe

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ametoa zile alizoita, hongera nyingi kwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, ambaye ameshinda muhula wa saba wa uongozi akiwa na umri wa miaka 89.
Zuma akikaribishwa na Mugabe alipozuru Harare zamani
Rais Zuma amesema uchaguzi mkuu wa Zimbabwe ulifanikiwa, na ametoa wito kwa pande zote zikubali matokeo.
Mpinzani mkuu wa Bwana Mugabe, Morgan Tsvangirai, mwenye umri wa miaka 61, amekataa matokeo na amesema atapeleka malalamiko mahakamani.
Viongozi wa mataifa ya magharibi yamesema yana wasi-wasi kama uchaguzi ulikuwa wa halali.
Bwana Mugabe alipata asili-mia-61 ya kura katika uchaguzi wa rais.
Na chama chake cha ZANU-PF kilipata thuluthi mbili ya viti vya bunge.

Gor Mahia yatoka sare na City Stars

Gor Mahia leo hii imetoka suluhu na City Stars huku Tusker ikishinda Chemilil Sugar bao 1-0 magharibi mwa Kenya kati ya mechi kadhaa za ligi kuu ya Kenya zilizochezwa leo.
Neymar aumwa
Neymar aumwa

Licha ya sare hiyo,Gor Mahia bado inaongoza ikiwa na pointi 37 ikifuatiwa na Thika United na AFC Leopards.
Leopards jana imeinyoa Ulinzi bao 1-0, mfungaji akiwa ni Allan Wanga alipounganisha krosi ya Charles Okwemba.
Muhoroni Youth ilishinda Sofapaka 1-0 na KCB ikaongeza machungu kwa Homeboyz ya magharibi mwa Kenya ilipoizaba mabao 2-1..
Katika habari za Kimataifa ingawa ni barani Afrika, Mbwana Samata amefululiza na mwendo mdundo wa kufunga katika kila mechi akiongoza na kuiweka kifua mbele Klabu yake ya TP Mazembe katika michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kuinyuka FUS Rabat ya Morocco bao 3-0.
Hadi mechi hio Mbwana mwenye umri wa miaka 21 kutoka Tanzania amefunga mara nne katika mechi nne ambapo Mazembe ikitafuta ufanisi.
Itakumbukwa kua Mbwana Samata amefunga katika mechi zote za nyumbani na ugenini dhidi ya Liga Muculmana ya Msumbiji kisha katika mchuano mwingine wa ufunguzi dhidi ya Entente Setif ya Algeria majuma mawili yaliyopita.
Ushindi wa Mazembe katika mji wa Lubumbashi dhidi ya washindi wa Kombe la shirikisho mwaka 2010 unaiweka Mazembe kwenye kilele cha Kundi B.
CA Bizertin ya Tunisia ilitizamiwa kupambana na Setif baadaye jumapili kwa mchuano mwingine wa kundi hili la B ingawa uwanja ulipanga kua chini ya ulinzi mkali kutokana na hali ya mbovu ya kisiasa inayopitia Mataifa ya Kiarabu.
Washindi wa kombe hili mnamo mwaka 2006 waliiondoa klabu ya St Geaoge kutoka Ethiopia 2-1 mjini Sousse.
Ushindi huo ulikua mgumu baada ya Mohamed Nafkha kujifunga bao mwenyewe lakini Issam Jbali alirudisha bao hilo kabla ya Baghdad Bounedjah kupata la ushindi katika kipindi cha pili.
Na hapa Ulaya Klabu ya Barcelona imetangaza kua mchezaji wao mgeni kutoka Brazil Neymar amepatikana kua na upungufu wa damu mwilini, ingawa hilo halitomzuia kuendelea na mazowezi.
Klabu hiyo imeongezea kusema kua Neymar alikumbwa na tatizo hilo la upungufu wa damu kufuatia operesheni ya findo au tonsilitis.
Maradhi haya ni kupungua kwa kipimo cha seli nyekundu za damu ambazo husababishia mgonjwa kujihisi mchovu au dhaifu mara kwa mara.