Jumatatu, 5 Agosti 2013

Don Jazzy aungana tena na D’Banj!

Don-Jazzy-Dbanj-pictured-at-Cool-FMs-Dotun-and-Taiwo-Oyebanjo-Ojuolape-wedding

Patna wa zamani wa Mo’Hits Records, Don Jazzy and D’Banj wameonekana pamoja kwa mara ya kwanza tangu waachane mnamo March 2012.
Patna hao walikutana katika harusi ya dada  mdogo wa D’Banj ambaye alifunga ndoa na Dotun wa Cool FM jana, August 3, 2013 kwenye ukumbi maarufu wa The Grandeur Event Centre uliopo Ikeja mjini Lagos.
Don Jazzy ambaye ni produza mkali wa Mavin Records na D’Banj ambaye ni msanii machachari kutoka DB Records waliwapagawisha wageni waalikwa baada ya kuivamia steji na kuanza kuwarusha maharusi kwa nyimbo zao kali za ‘Mr Endowed‘, ‘Fall in love‘ and ‘Suddenly‘.
Japokuwa patna hao walishawahi kukutana mara kadhaa tangu waachane, hii ilikuwa ni mara yao ya kwanza kuimba pamoja stejini tangu walipoachana.
D’Banj alielezea furaha yake ya kuungana tena na Jazzy pia aliwapa maharusi zawadi ya gari mpya na ya kisasa aina ya Honda CRV.
Uhusiano wa kimuziki wa Don Jazzy na D’banj ulivunjika bila ya kujulikana chanzo cha mgogoro huo mnamo mwaka jana.Watu waliokuwa lebo moja na washiriki kama Dr SID, D’Prince na Wande Coal walijiunga upande wa Don Jazzy wakati mdogo wake, KaySwitch alijiunga na D’Banj.

Jumamosi, 27 Julai 2013

NILIJUA TU KWAMBA WANAFIKI WATAFURAHIA MATESO YANGU" ....AGNESS MASONGANGE


VIDEO Queen ambaye hivi karibuni alidaiwa kukamatwa na madawa yanayosadikiwa ni ya kulevya ‘unga’ nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’, Agness Gerald ‘Masogange’ amefunguka kuwa alijua watu wengi watafurahia kilichompata kwa kumuongelea kila wakati.
Akizungumza na mwanahabari wetu kwa njia ya simu akiwa Sauzi, Masongange ‘alishauti’ kuwa watu wengi wanamuongelea vibaya bila kujua nini kilichompata  hivyo anaamini hata marafiki zake wa karibu wamefurahia tatizo alilopata.

“Najua kabisa kuna watu wengi wamefurahia tatizo nililopata lakini watambue kuwa kila mtu anaweza kupata tatizo hivyo wapunguze kuongea sana bila kujua ni kitu gani kilichotokea juu yangu,” alisema Masogange ambaye atapanda kizimbani kwa mara ya pili mwezi ujao

UPDATE: Baada ya tuhuma, hatimaye Jennifer Kyaka (Odama) atoa ushahidi wa kwenda nje.

UPDATE: Baada ya tuhuma, hatimaye Jennifer Kyaka (Odama) atoa ushahidi wa kwenda nje.
  • UPDATE: Baada ya tuhuma, hatimaye Jennifer Kyaka (Odama) atoa ushahidi wa kwenda nje. 1
  • UPDATE: Baada ya tuhuma, hatimaye Jennifer Kyaka (Odama) atoa ushahidi wa kwenda nje. 2
  • UPDATE: Baada ya tuhuma, hatimaye Jennifer Kyaka (Odama) atoa ushahidi wa kwenda nje. 3
Baada ya wadau mbalimbali kuanza kuhoji kuhusu uhalisia wa safari za mwigizaji Jennifer Kyaka (Odama) kwenda ulaya ambaye picha zake kadhaa zilizotolewa mtandaoni wiki chache zilizopita zikimtuhumu kuwa huwa haendi nje ya nchi bali anakuwepo nchini kwa lengo la kutafuta “kiki” na kutengezeza picha hizo kwa program maalumu ya kompyuta, hatimaye jana kupitia mtandao mmoja wa kijamii aliweka picha zake mpya zinazomuonesha nchini Qatar katika maduka mbalimbali na kwenye uwanja wa ndege wa nchi hiyo.
 Picha hizi zimekuja kama ushahidi na majibu ya mwaswali yaliyokuwa yakiulizwa na wadau wengi kuhusu mwanadada huyu. Tazama picha hizi hapo

PICHA: Kajala masanja akiwa afrika ya kusini, atembelea shule ya uigizaji

PICHA: Kajala masanja akiwa afrika ya kusini, atembelea shule ya uigizaji
  • PICHA: Kajala masanja akiwa afrika ya kusini, atembelea shule ya uigizaji 1
  • PICHA: Kajala masanja akiwa afrika ya kusini, atembelea shule ya uigizaji 2
  • PICHA: Kajala masanja akiwa afrika ya kusini, atembelea shule ya uigizaji 3
  • PICHA: Kajala masanja akiwa afrika ya kusini, atembelea shule ya uigizaji 4
Juzi mwigizaji wa bongo movies  Kajala aliondokoka nchini kuelekea Afrika ya kusini kwa ajili ya safari binasfi ambayo pamoja na mambo mengine alitembelea  shue ya uigizaji ya AFDA (AFDA the South African School of Motion Picture Medium and Live Performance)  iliyopo nchini humo.
Tazama hapo picha kadhaa za msanii huyo nchini humo

Wakazi ajibu “diss” ya TID

wakazi
Baada ya TID kuandika:
“Wakazi ataimba wimbo gani, anaenda kuonyesha kofia zake za marekani#mzee kasema#radarworththisshit#watuwabaya#msiwemaf**a.”
katika mtandao wa Twitter kufuatia Wakazi kualikwa kuperform katika eviction show ya Big Brother Africa, Wakazi amemjibu kwa kusema:
“Sasa ntamjibu nini, anaongea vitu asivyovifahamu, yeye hapo akimuona Wakazi anaona kofia za Marekani sasa mtu kama huyo utaongea naye? The greatest ignorance ya mtu ni pale anapoamua kudiss kitu ambacho hakijui au hajakifahamu bado vizuri , mtu kama huyo huwezi kuanza kubishana naye, na yeye ananiona mimi Mmarekani, wakati mimi ni Mtanzania, angekaa miaka mitatu Ulaya au Marekani angejiona na yeye ni mtu wa huko kwa jinsi upeo wake ulivyo.”

Majina ya askari saba wa Tanzania waliokufa kwenye shambulio la ghafla mjini Darfur

jem-force
Majina ya askari saba wa Tanzania waliokufa kwenye shambulio la ghafla mjini Darfur yamepatikana.
Askari hao waliokufa ambao walikuwa kwenye vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa huko nchini Sudan ni Sajenti Shaibu Othuman, Koplo Oswald Chaula, Koplo Mohamed Juma, Koplo Mohamed Chikilizo, Pte. Rodney Ndunguru, Pte. Peter Werema na Pte. Fortunatus Msofe.
Taarifa zilizopatikana kwenye mtandao ni kwamba askari hao walikwenda kujaribu kumwokoa mwenzao (ambaye hakutajwa) ambaye alisemekana kutekwa na vikosi vya waasi nchini humo.Wakati wakijiandaa, ghafla walizingirwa na askari hao waasi na kisha kushambuliwa kwa risasi hadi kufa.
Haikufahamika hali ya askari huyo ambaye alidaiwa kutekwa kama bado yu hai ama ni miongoni mwa waliokufa.
Mungu azilaze roho za askari wetu mahali pema peponi, Amina.

Hot: Waraka wa Kala Jeremiah kuhusu Mh. Edward Lowassa

Kala-Jeremiah
TANGAZO KWA UMMA
MIMI KALA JEREMIAH NILIKUWA MSANII WA KWANZA TANZANIA KUMSEMA MHESHIMIWA EDWARD LOWASA KUPITIA WIMBO WANGU UITWAO WIMBO WA TAIFA BAADA YA MHESHIMIWA KUKUMBWA NA KASHFA YA UFISADI WA RICHMOND.KWA KIPINDI KILE KILA MMOJA WETU ALIHAMAKI SANA NA KUONA KWELI MZEE WA WATU NI FISADI.KWENYE WIMBO HUO KUNA MISTARI NILISEMA. mi siyo mwana siasa sisubiri tume ichunguze nistaafu ka Lowasa.
KWA KUWA MIMI NI MZURI SANA KWENYE KUFANYA UCHUNGUZI BINAFSI NILITUMIA MUDA MWINGI SANA KULICHUNGUZA SWALA HILI LA KASHFA HII NA BAADAE NILIGUNDUA KUWA NI SWALA LA KISIASA.NA YALIKUWA NI MAPITO AMBAYO MWANADAMU YOYOTE HUPEWA MUDA WA KUPITIA MAGUMU ILI KUPIMWA IMANI YAKE KWA MUNGU.
BAADA YA KUGUNDUA HAYO MWAKA JANA NILITENGENEZA WIMBO UNAOITWA AZIMIO LA ARUSHA AMBAO UPO KWENYE ALBUM YANGU YA PASAKA AMBAYO IKO SOKONI TOKEA MWAKA JANA. KATIKA WIMBO HUO WA AZIMIO LA ARUSHA NILIANDIKA MISTARI IFUATAYO. walipiga dili waka msakizia lowasa ili kuficha siri kali.NILIANDIKA MSTARI HUU BAADA YA KUFANYA UCHUNGUZI NA KUJIRIDHISHA KUWA MHESHIMIWA NI KIONGOZI BORA SANA NA HASA KWA UAMUZI WAKE WA KUJIUZULU BILA SHINIKIZO KUBWA NA WAKATI KWA NAFASI ALIYOKUWA NAYO YA UWAZIRI MKUU ALIKUWA NA UWEZO WA KUGOMA KUJIUZULU NA HASA KWA KUWA HAKUWA FISADI KAMA ILIVYOSEMWA.
MWEZI WA TATU MWISHONI MWAKA HUU NILITOA WIMBO UNAOKWENDA KWA JINA LA KARIBU DAR AMBAKO NILISEMA dar es salam ingekuwa nchi Rais angekuwa Lowasa huku watu washashtukia kuna mchezo kwenye siasa HAPA NILIKUWA NAMAANISHA KUWA WATU WENGI WANAOISHI DAR WANAWAHI KUJUA MAMBO YA WANASIASA KWA KUWA WANASIASA WANAISHI HUKU LAKINI PIA WATAFITI WENGI WA MAMBO YA KISIASA WANAISHI HUKU KWA HIYO NI RAHISI ZAIDI KUUJUA UKWELI MAPEMA.
NAAMINI KUONDOKA KWA LOWASA KWENYE UWAZIRI MKUU KUMEZOROTESHA MAENDELEO YA TAIFA KWA KIASI FLANI
NDUGU ZANGU WATANZANIA NI WAZI KUWA LOWASA NI JEMBE TENA JEMBE LA KAZI KUMBUKENI BILA LOWASA KUSINGEKUWA NA SHULE ZA KATA TANZANIA,NA ANGEENDELEA KUWEPO MADARAKANI ALIKUWA NA MPANGO WA KUANZA MCHAKATO WA ZAHANATI ZA KATA.IKUMBUKWE PIA LOWASA NDIYE ALIYESIMAMIA UJENZI WA CHUO CHA UDOM TENA KWA PESA ZA KITANZANIA BILA KUOMBAOMBA VIMIKOPO.
MRADI WA MAJI KUTOKA MWANZA KWENDA SHINYANGA NI KAZI YA LOWASA. ZIPO KAZI NYINGI AMBAZO NIKIZITAJA ZOTE NAWEZA KUJAZA UKURASA.NACHOJARIBU KUSEMA HAPA NI KWA KUWA MIMI NI MSANII NA NI KIOO CHA JAMII NINGEOMBA WEWE MWANAJAMII CHUKUA HATUA YA KUFANYA UCHUNGUZI BINAFSI KUHUSU LOWASA.BILA KUFUATA MKUMBO WA KISIASA NAAMINI UTAKUBALIANA NA MIMI KUWA LOWASA NI JEMBE.
MIMI HUWA NAPENDA KUSOMA VITABU VYA WANAHARAKATI NA KUNA KITABU KIMOJA NILIKIPITIA CHA MWANAHARAKATI KUTOKA ITALY AITWAE NICCOLO MACHIAVELLI AMBAYE ALIZALIWA MWAKA 1469 NA KUFARIKI 1527. KATIKA ENZI ZA UHAI WAKE ALIWAHI KUANDIKA VITABU KADHAA LAKINI KATI YA VITABU HIVYO KITABU KIITWACHO THE PRINCE NDICHO KILIMPA HESHIMA KUBWA SANA KWA KUWA ALIIKOSOA SERIKALI YA KIFALME YA KIPINDI HICHO KITU AMBACHO HAKIKUWA RAHISI KWA MTU KUFANYA HASA IKIKUMBUKWA KUWA ENZI ZA UFALME ZILIKUWA ENZI ZA UBABE. KATIKA MANENO KUTOKA KWENYE KITABU HICHO AMBAYO NINGE PENDA KUKUSHIRIKISHA WEWE NDUGU YANGU MTANZANIA NI MANENO YAFUATAYO MACHIAVELLI ALIANDIKA HIVI. kuna kipindi ambacho mataifa yanapita katika vipindi vigumu. na kwa kipindi hicho kigumu mataifa hayo yatahitaji sana kupata kiongozi mwenye kuweza kuchukua maamuzi magumu,na ambaye hatakuwa chini ya sauti ya mtu mwingine, na ambaye ataweza kuyatekeleza maamuzi magumu kwa haraka hata kama ni kwa kuwaumiza wachache ili wengi wawe huru.atakayekuwa tayari kutekeleza jambo baya ili likapita na kusahaulika na atakayetekeleza mambo mazuri kwa muda mrefu na yakaendlea kukumbukwa.kiongozi huyo atatakiwa kuchagua kuogopwa ama kupendwa lakini ni bora akachagua kuogopwa lakini akitenda haki kwa wananchi husika.HAYO NI BAADHI YA MANENO ALIYOANDIKA MACHIAVELLI KWENYE THE PRINCE KITABU AMBACHO KILIMPELEKEA KUITWA NA MFALME NA KUPEWA NAFASI YA JUU YA UONGOZI KATIKA SERIKALI HIYO YA KIFALME.
KWA MAONI YANGU NADHANI TAIFA LETU LIMEPITIA VIPINDI VIGUMU KADHAA NA KWA MANENO YA BWANA MACHIAVELLI NADHANI KIONGOZI ANAYEFAA AMBAYE ANAWEZA AKACHUKUA MAAMUZI MAGUMU NA AMBAYE HAWEZI KUWA CHINI YA SAUTI YA MTU MWINGINE NI MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASA.