Mkongwe wa muziki, Janet Jackson, ajipatia nafasi kwenye klabu ya mabilionea kupitia mauzo na shoo za albamu zake kali na kushiriki katika filamu mbalimbali.
Kutoka katika chati za muziki mpaka kwenye fashion, hajawahi kushindwa kuonekana kwa njia moja au nyingine.
Sasa, Janet Jackson ameongezwa kwenye orodha nyingine: mabilionea.
Kwa mujibu wa Variety Magazine, Jackson amejipatia dola milioni 458 kutoka kwenye ziara za muziki na dola milioni 260 kutokana na mauzo ya albamu zake.Vilevile alipokea dola milioni 81 kutoka kwa wadhamini na dola milioni 304 kutoka kwenye uigizaji filamu mbalimbali.
Mwaka jana (2012), alifunga ndoa na bilionea Wissam Al Man kwa siri.
Jackson anaungana na mastaa wengine maarufu na mabilionea wa Hollywood kama vile Oprah Winfrey, steven Spielberg, J.K. Rowling and Sara Blakely.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni