Watoto mapacha wa kiume wamezaliwa huko India wakiwa na vichwa viwili katika mwili mmoja kitu ambacho inasemekana ni nadra sana kutokea.
Madaktari
wamesema wanaamini wanauwezo wa kuokoa maisha ya watoto hao ambao
wamezaliwa Jumatano (July 24) huko Jaipur, Rajasthan India.
Kwa mujibu wa taarifa ya Daily Mail, nervous system ya watoto hao imetengana wakati uti wa mgongo umeungana na pia wanashare sehemu ya ubavu.
Dr.
S.D. Sharma, wa J.K. Lone Hospital amesema tatizo kama hilo ni nadra
sana kutokea hususan kwa watoto wa kiume, na linafahamika kama
‘Dicephalic Parapagus’. Aliongeza kuwa tukio hilo ni la pili kutokea
India.
Daktari
huyo aliendelea kusema kuwa mara nyingi watoto wenye ‘Dicephalic
Parapagus’ huzaliwa wakiwa wamekufa, na mara nyingi hutokea kwa watoto
wa kike. Kwa mujibu wa Sharma alisema kuna uwezekano wa kuokoa maisha ya
mapacha hao.
Tatizo
kama hilo lililowahi kutokea kwa mapacha wa kike kutoka Sudan mwaka
(2011) ambao waliozaliwa wakiwa wameungana vichwa. Watoto hao Rital na
Ritag Gaboura walifanikiwa kutenganishwa salama japo kwa tatizo kama lao
uwezekano wa kupona hua ni kwa mmoja kati ya million kumi
Rital na Ritag Gaboura wa Sudan baada ya kutenganishwa
Inasemekana tatizo la mapacha kuzaliwa wameungana hutokea mara moja kati ya watoto 100,000 wanaozaliwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni