Mashirika ya misaada yanataka UN kujali hali ya raia wakati mgogoro DRC ukiendelea
Mashirika ya misaada katika
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo , yameelezea hofu kuhusu operesheni ya
kijeshi inayopangwa na Umoja wa Mataifa yakisema kuwa itavuruga zaidi
hali ya kibinadamu nchini humo.
Mashirika hayo yanayoshughulikia wakimbizi
yanasema kuwa umoja wa mataifa unastahili kutumia mbinu salama zaidi ili
kuwaokoa raia kutokana na athari za hatua ya kikosi cha Umoja huo
kuingilia kati mzozo unaoendelea.Tayari wanajeshi wameanza kushika doria
Shirika la misaada la Medecins Sans Frontieres hapo awali lililalamika kuwa kuwepo kwa vikosi vya UN kunaweza kutatiza shughuli za shirika hilo kuwapa msaada waathiriwa wa mgogoro huo kwani huenda wakalengwa kwa mashambulizi na wapiganaji.
Baraza la umoja wa mataifa baadaye leo litajadili hali nchini DRC ambako zaidi ya watu milioni mbili unusu wameachwa bila makaazi kutokana na mzozo huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni